NDEGE aina ya tandawala machaka(Denihams bustard) pichani wenye uwezo wa kuruka toka Bara moja hadi jingine inaaminika wanapumzika katika misitu ya Hifadhi ya asili ya Ruhekei na Liwilikutesa wilayani Nyasa Mkoa wa Ruvuma.
Afisa Maliasili na Utalii wa mkoa wa Ruvuma Africanus Challe anasema hali ya hewa iliyopo katika miinuko ya misitu ya Ruhekei na Liwilikutesa inafanana na ya Hifadhi ya Taifa ya kitulo hali ambayo inasababisha ndege hao adimu duniani kupumzika katika misitu ya Nyasa.Hifadhi ya misitu ya asili ya Ruhekei yenye ukubwa wa zaidi ya hekta 2000 ilianzishwa kwa kutangazwa katika gazeti la serikali ya kikoloni mwaka 1938 na Liwilikitesa ni msitu wa asili unaohifadhiwa na serikali kuu ambao ulitambulika tangu mwaka 1950 wakati wa utawala wa kikoloni.Mhifadhi toka Hifadhi ya Taifa ya Kitulo Godfrey Kyando anasema ndege hao wanafika kwa ajili ya kutaga na kuangua vifaranga katika Hifadhi ya Taifa ya Kitulo iliyopo wilayani Makete Mkoa wa Njombe kuanzia Machi hadi Julai kila mwaka kisha wanaruka na kwenda katika maeneo mengine duniani ambapo uchunguzi umebaini ndege hao wanapumzika maeneo ya Nyasa na kisha kuendelea na safari ya kutoka bara moja hadi jingine.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa