KESHO ni Jumamosi Mei 26,2018,Jumamosi ya mwisho wa mwezi ambayo ni siku ya kitaifa ya usafi wa mazingira kila mmoja ashiriki kikamilifu.Serikali imepitisha sheria rasmi kuanzia mwaka 2016, kila Jumamosi ya mwisho wa kila mwezi itakuwa siku ya usafi wa mazingira kwa nchi nzima.Ili kuhakikisha kuwa magonjwa yanayotokana na uchafu kama kipindupindu hayaendelei kuangamiza maisha ya watanzania, Wizara ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano imeagiza kila mwananchi atawajibika kufanya usafi wa mazingira wa eneo lake ifikapo kila Jumamosi ya mwisho wa kila mwezi na kwamba watendaji watakaoshindwa kusimamia zoezi hili watawajibishwa mara moja kwa mujibu wa sheria.
BOFYA HAPA USAFI WA MAZINGIRA.jpg
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa