Kamati ya fedha na uongozi Manispaa ya Songea ikiongozwa na Mstahiki Meya Manispaa ya Songea Michael Mbano, wamefanya ziara ya kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo iliyopo kwenye kata Manispaa ya Songea.
Ziara hiyo imefanyika tarehe 28 aprili 2021 kwa lengo la kufanya ufuatiliaji wa fedha zilizotolewa na Serikali kama zimetumika ipasavyo.
Miongoni mwa miradi iliyotembelewa na kamati ya fedha ni pamoja na ujenzi wa bwalo Sekondari ya Emmanuel Nchimbi, ujenzi wa bweni mdandamo Sekondari, ujenzi wa soko la mahindi msamala, madarasa 3 shule ya msingi bombambili, ukarabati wa stendi ya Ruhuwiko, ujenzi wa madarasa mawili mateka Sekondari, pamoja na ujenzi wa darasa moja shule ya msingi Changarawe nk.
AMINA PILLY;
AFISA HABARI MANISPAA SONGEA.
29.04.2021
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa