Na,
AMINA PILLY,
AFISA HABARI MANISPAA.
06 Mei, 2022
Kamati ya fedha na uongozi ya Halmashauri ya Manispaa ya Songea imefanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Halmashauri hiyo leo tarehe 6 Mei 2022.
Akizungumza katika ziara hiyo, Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Michael Mbano alisema kuwa, lengo la kufanyika kwa ziara hiyo ni kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ili kuchochea kasi ya ukamilishwaji wa miradi hiyo pamoja na kutatua changamoto zinazojitokeza katika zoezi la ukamilishwaji wa miradi mbalimbali.
Katika ziara hiyo kamati ya fedha na uongozi imeweza kukagua jumla ya miradi nane ambayo ni pamoja na ujenzi wa kituo cha afya Subira unaogharimu Tsh. 500,000,000 zitokanazo na fedha za tozo, ujenzi wa kituo cha afya Lilambo unaogharimu Tsh. 500,000,000 fedha kutoka mapato ya ndani, ujenzi wa miundombinu ya maji shule ya msingi Ruhuwiko (mradi wa EP4R) Tsh. 11,872,379 na ujenzi wa zahanati ya Ruhuwiko unaogharimu Tsh. 50,000,000 fedha kutoka Serikali kuu.
Kamati imetembelea mradi wa ujenzi wa madarasa 3 shule ya msingi Mkuzo (mradi wa Tea) Tsh. Million 60,000,000, ujenzi wa madarasa 8 Ruhila Sekondari unaogharimu Tsh. 470,000,000 mradi wa SEQUIP, ujenzi wa madarasa 3 shule msingi Ruhilaseko (mradi wa Tea) Tsh. 60,000,000 pamoja na ujenzi wa matundu 24 ya vyoo shule ya msingi Matogoro unaogharimu Tsh. 40,000,000 (mradi wa Tea) ambapo kamati imeridhishwa na utekelezaji wa miradi hiyo.
Mwisho.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa