Kamati ya fedha na uongozi Manispaa ya Songea kwa kushirikiana na wataalamu imeweka mpango mkakati wa kuboresha ukusanyaji wa mapato ya ndani kupitia vyanzo vyake vya mapato kwa lengo la kuongeza tija ya ukusanyaji wa mapato katika Halmashauri.
Kauli hiyo imebainishwa leo tarehe 20 Oktoba 2022 wakati wa ziara ya kamati ya fedha na uongozi iliyofanyika kwa lengo la kujiridhisha na kukagua hatua mbalimbali za utekelezaji wa miradi ya ujenzi, na kutembelea vyanzo mbali mbali vya mapato hususani chanzo cha madini ya ujenzi.
Ziara hiyo ya siku moja ambayo imeongozwa na mstahiki Meya Manispaa ya Songea Michael Mbano ambaye amewataka wataalamu kuwa wabunifu katika kuibua vyanzo vipya vya mapato ambavyo vitawezesha kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato.
Kamati ya fedha na uongozi imetembelea mradi wa kituo cha afya Mletele unaotekelezwa kwa gharama ya shilingi 545,334,640, ujenzi wa mabweni 2 na vyumba 3 madarasa ya shule ya sekondari ya wavulana Songea kwa gharama ya Mil. 260, ujenzi wa bweni 2 na vyumba vya 4 vya madarasa shule ya Sekondari wasichana Songea kwa gharama ya shilingi Mil. 280, eneo la ujenzi wa Holding Ground pamoja na kutembelea chanzo cha madini ya ujenzi.
Naye Mchumi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Andambike Kyomo akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea alisema Manispaa ya Songea imekusudia kukusanya kiasi cha shilingi Mil. 151,200,000 kupitia vyanzo vya madini ya ujenzi ambapo kuanzia julai hadi tarehe 20 Oktoba 2022 Manispaa ya Songea tayari imekusanya kiasi cha shilingi Mil. 10,200,000 na zoezi linaendelea.
AMINA PILLY
KITENGO CHA MWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa