Kamati ya fedha na uongozi ikiongozwa na Mstahiki Meya Manispaa ya Songea Mheshimiwa Michael Mbano amefanya ziara ya kutembelea miradi ya Maendeleo iliyofanyika leo tarehe 07 Februari 2024 kwa lengo la kukagua hali ya utekelezaji wa miradi hiyo.
Miongoni mwa miradi iliyotembelewa ni pamoja na ujenzi wa ofisi ya kata Mjini iliyojengwa kwa thamani ya Mil.20 fedha za mapato ya ndani ambapo ujenzi huo upo hatua ya ukamilishaji, Ujenzi wa shule mpya Chief Zulu Academy iliyojengwa kwa gharama ya mil. 491,2 fedha za mapato ya ndani ambapo Ujenzi huo umekamilika na shule imefunguliwa, ujenzi wa sekondari ya Dkt. Lawrance Gama iliyojengwa kwa thamani ya Mil. 560 fedha za SEQUIP ambayo imekamilika na imefunguliwa, pamoja na ukaguzi wa kikundi cha mradi wa vifungashio kilichojengwa kwa Mil 229 fedha za mapato ya ndani.
Akizungumza Mstahiki Meya Manispaa ya Songea Michael Mbano amewataka wataalamu wote kuhakikisha wanasimamia miradi kwa weredi na kukamilisha kwa wakati.
IMEANDALIWA NA,
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa