KAMATI ya Fedha na Uongozi ya Baraza la Madiwani la Manispaa ya Songea imefanya ziara ya kukagua na kufanya tathmini ya miradi ya maendeleo iliyopo katika manispaa ya Songea.
Moja ya miradi hiyo ni ujenzi wa bustani ya Manispaa ya Songea, mradi ambao unagharimu sh.milioni 399 kwa ufadhili wa Benki ya Dunia.Mradi huo una eneo la mgahawa, choo cha kulipia, uzio na maeneo ya kupaki magari, bustani hiyo pia ina eneo la kupumzikia ( resting huts ) ,maeneo ya kuchezea watoto, hoteli,eneo ambalo lina mnara na bustani ya nyasi na miti.
Mradi upo katika hatua za mwisho. Kamati imeridhishwa na hatua ya ujenzi wa mradi wa bustani hiyo ambao ni wa miezi sita, ulianza Machi 2017 na ulitarajiwa kukamilika Septemba 30,2017.
Imetolewa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa