Kamati ya fedha na Uongozi Manispaa ya Songea ikiongozwa na Naibu Meya Mhe. Jeremia Mirembe wamefanya ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo pamoja kukagua utendaji wa kazi na kujionea hali halisi ya utekelezaji wa miradi hiyo.
Ziara hiyo imefanyika leo tarehe 14 Agosti 2023 ambayo ilishirikisha waheshimiwa Madiwani wa kamati ya fedha na uongozi, pamoja na wataalamu kwa lengo la kukagua miradi ya BOOST ambayo ipo hatua ya ukamilishaji.
Akizungumza Mhe. Jeremia kwaniaba ya Mstahiki Meya Manispaa ya Songea alianza kwa kuwapongeza wataalamu wote kwa usimamizi bora wa miradi ya maendeleo ambapo amewataka wataalamu kuhakikisha wanaendelea kusimamia miradi hiyo na kukamilisha kwa wakati.
Miongoni mwa miradi iliyotembelewa ni pamoja na ujenzi wa shule ya Msingi Kipera kwa gharama ya Mil 513, ujenzi wa madarasa matatu na matundu 3 ya vyoo kwa shule ya Msingi Mbulani kwa gharama ya Mil 77, Ujenzi wa madarasa 2 katika shule ya Msingi Matogoro kwa gharama ya Mil. 53, Ujenzi wa Madarasa mawili shule ya Msingi Bombambili kwa gharama ya Mil. 53, Ujenzi wa madarasa 2 na matundu 3 ya vyoo shule ya Msingi Mkuzo kwa gharama ya Mil. 53 Ujenzi wa Vyumba 10 vya madarasa, mabweni 4, na matundu ya vyoo 15 katika shule ya Sekondari Emmanuel Nchimbi kwa gharama ya Mil. 777, Ujenzi wa madarasa 3 na matundu 3 ya vyoo katika shule ya Msingi Ruhuwiko kwa gharama ya Mil. 77, pamoja na ujenzi wa Madarasa 2 ya awali katika shule ya Msingi Amani kwa gharama ya Mil. 66 ambapo ujenzi wote upo hatua ya Ukamilishaji.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa