Kamati ya fedha na Uongozi Manispaa ya Songea imefanya ziara ya kutembelea miradi ya Maendeleo kwa lengo la kufanya ukaguzi wa miradi inayotekelezwa katika Halmashauri na kuthaminisha hali ya mradi na thamani ya fedha iliyotolewa.
Kamati hiyo iliongozwa na Mstahiki Meya Manispaa ya Songea Michael Mbano iliyofanyika jana tarehe 18 Januari 2023 na kufanikiwa kutembelea miradi wa ujenzi wa uzio wa Bweni la watoto wenye mahitaji maalmu kata ya Subira kwa fedha Mil. 60 kutoka Serikali kuu, ukamilishaji wa Bweni Sekondari ya Chabruma kata ya Lilambo kwa fedha Mil 22 kutoka Serikali kuu, ukamilishaji wa madarasa mawili Shule ya Msingi Sabasaba fedha Mil. 25 kutoka Serikali kuu, kukagua miradi ya barabara za mitaa za kata ya Bombambili na Msamala kwa thamani ya Mil. 20,000 kwa kila kata fedha za mapato ya ndani, Ukamilishaji wa Bweni Mdandamo Sekondari kwa fedha Mil 38 kutoka Serikali kuu pamoja na kukagua mradi wa kivuko kata ya Mletele Mil 20 kwa fedha za mapato ya ndani.
Mhe.Mbano alianza kwa kuwapongeza wataalamu kwa kutoa fedha mil. 20 fedha za mapato ya ndani kupeleka kwenye kila Kata kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ambayo imekuwa ni adha katika kata husika ambapo katika kutekeleza agizo hilo kata 3 za awali ambazo ni kata ya Bombambili, kata ya Msamala, na Mletele zimeshapokea fedha hizo na utekelezaji wa kazi umeshakamilika. “Amepongeza“
Alibainisha kuwa kata ya Bombambili imepokea fedha Mil 20 imetumika kutengeneza barabara za mitaa, kata ya Msamala imepokea fedha Mil. 20 ambazo zimetumika kwa ajili ya utengenezaji wa kivuko Mtaa wa Mtaungana ambapo imesaidia kutatua changamoto ya kivuko kuelekea Kata ya Mjimwema na ujenzi wa kivuko kata ya Mletele. “ Mhe. Mbano alibainisha.”
Hata hivyo kamati ya fedha na uongozi ilipongeza jitihada za wataalamu kwa kusimamia vizuri miradi ya maendeleo ambapo wametoa rai kwa wataalamu kuendelea kutoa ushirikiano katika kusimamia na kutekeleza miradi ya maendeleo ya Halmashauri.
Akitoa shukrani kwa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini ambaye pia ni Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro kwa kutoa fedha za miradi mbalimbali ambayo inaendelea kutekelezwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea ikiwemo na fedha za ujenzi wa madarasa 76 ambayo kwasasa yamekamilika na watoto wameingia darsani. "Mstahiki Meya alishukuru".
Kwa upande wake Afisa Mtendaji kata ya Msamala Deogratias Chaima alisema kuwa katika kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2022/2023 kata ya Msamala imepokea shilingi Mil. 20 kutoka kwa Mkurugenzi Manispaa ya Songea fedha za mapato ya ndani ambazo zimetumika kutengeneza kivuko na bara bara za mitaa KM. 7.9.
Imeandaliwa na;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa