KAMATI ya Fedha na Uongozi ya ya Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Songea imefanya ziara ya kukagua miradi iliyotekelezwa katika robo ya pili.
Miradi iliyokaguliwa ni ujenzi wa machinjio ya kisasa katika kata ya shule ya Tanga unaogharimu zaidi ya shilingi bilioni tatu ambao umefikia asilimia 40 ya ujenzi.Mradi huo unatarajia kukamilika Juni 2018.
Miradi mingine ni ujenzi wa madarasa matano na matundu 12 ya vyoo katika shule ya msingi Majimaji unaogharimu milioni 66.6 na mradi wa ujenzi wa madarasa matano na matundu 12 ya vyoo katika shule ya msingi Kipera ambao unaogharimu milioni 61.
Kamati imeridhishwa na ujenzi wa Miradi yote isipokuwa katika mradi wa vyumba viwili vya madarasa katika shule ya msingi Changarawe kata ya Mletele ambapo hali ya ujenzi hairidhishi wanafunzi wanasomea katika madarasa ambayo hayana sakafu na wengine wanasomea chini ya Miti.
Mchumi Mkuu wa Manispaa ya Songea Kimary amesema Manispaa kupitia mapato ya ndani imetoa shilingi milioni 22 kwa ajili ya ujenzi wa matundu 12 ya vyoo na vyumba viwili vya madarasa ambavyo ujenzi wake umefikia zaidi ya asilimia 60.
Amesema katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2017/2018 kupitia mapato ya ndani Halmashauri ya Manispaa ya Songea imetenga shilingi milioni 127 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na vyoo katika shule 12 ikiwemo na shule ya msingi Changarawe.
Kamati imeagiza marebisho yafanyike haraka katika shule ya msingi Changarawe ili watoto wasiendelee kusomea nje kwa kuwa hali hiyo inaitia haibu Manispaa ya Songea.
Takwimu zilizotolewa na Mkuu wa wilaya ya Songea Pololet Mgema wakati anazungumza na madiwani wa Manispaa ya Songea hivi karibuni zinaonesha kuwa Manispaa ya Songea inakabiliwa na upungufu wa vyumba 500 vya madarasa kwa shule za msingi.
Sera ya elimu bure imepata mafanikio makubwa ya kuandikisha idadi kubwa ya wanafunzi hali inayoleta Changamoto katika vyumba vya madarasa katika shule za msingi na sekondari.
Imetolewa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa