Kamati ya fedha na Uongozi Manispaa ya Songea ikiongozwa na Naibu Meya Manispaa ya Songea Jeremia Mlembe wamefanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo kwa lengo la kufanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi hiyo.
Ziara hiyo imefanyika jana tarehe 08 Novemba ambapo wametembelea miradi ya ukarabati wa madarasa Shule ya Msingi matogoro, ukarabati wa madarasa Shule ya Msingi Songea, ukarabati wa madarasa Shule ya Msingi Majengo, Ujenzi wa shule ya Chief Zulu Academy inayojengwa kwa gharama ya Mil. 500 fedha za mapato ya ndani, na ujenzi wa shule ya Sekondari ya Lawrence Gama inayojengwa kwa fedha za Serikali kuu Mil. 500.
Mhe. Jeremia amewataka wataalamu kuendelea kushirikiana katika kusimamia ujenzi wa miradi ya maendeleo na kufikia lengo la Serikali lililokusudiwa.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa