Mwenyekiti wa kamati ya Lishe Manispaa ya Songea amewataka wataalamu wa Lishe, kuhakikisha wanaendelea kutoa elimu ya lishe kwa jamii ili kuondoa utapiamlo kwa watoto chini ya miaka 5 ambao katika kipindi cha Aprili hadi Juni ni watoto 13 sawa na asilimia 0.1% za watoto wenye utapiamlo mkali.
Takwimu hiyo imekuja mara baada ya kufanya uchunguzi wa hali ya lishe kwa kutumia mzingo wa mkono kwa watoto chini ya miaka 5 ambapo jumla ya watoto 33, 755 wenye umri chini ya miaka 5 walichunguzwa hali ya lishe kati ya 32,216 ambayo sawa na asilimia 104.7.9%, pia kati ya hao 13 waligundulika kuwa na utapiamlo mkali sawa na asilimia 0.1%.
Aidha jumla ya watoto 1257 ambao ni sawa na 3.7% walichunguzwa na waligundulika kuwa na utapiamlo wa kadiri, pia watoto 32485 walichunguzwa sawa na asilimia 96.2 hawakuwa na utapiamlo.
Kikao hicho kimefanyika leo tarehe 14 Septemba 2023 katika ukumbi wa Manispaa ya Songea kwa lengo la kufanya tathimini ya utekelezaji wa shughuli za lishe katika kipindi cha Aprili hadi Juni 2023.
Akizungumza Afisa Elimu Sekondari Bi. Janeth Moyo kwa niaba ya Mkurugenzi Manispaa ya Songea ambapo amewataka wakuu wa shule kuhakikisha wanazisimamia klabu za lishe za shule ili utekelezaji wa shughuli za lishe uweze kutekelezeka kwa usahihi.
Imeandaliwa na;
Amina Pilly;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa