Kamati ya lishe ya Manispaa ya Songea imeandaa mapendekezo ya awali ya mpango na bajeti wa mwaka 2024/2025 ambao umelenga kutatua changamoto mabalimbali za lishe katika manispaa ya Songea.
Akizungumza Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya Songea Bi Janeth Moyo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea, ambapo amezitaka idara na vitengo kuhakikisha zinatenga bajeti ya lishe kwa watumishi wenye mahitaji maalumu.
Kikao hicho kimefanyika tarehe 28 Novemba 2023 katika ukumbi wa Mkuu wa Wilaya ya Songea ambacho walihudhuria wataalamu wa afya, wajumbe kutoka idara ya Elimu, Kilimo na mifugo kwa lengo la kupitisha mapendekezo ya mpango na bajeti 2024/2025.
Imeandaliwa;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKLINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa