NA,
AMINA PILLY,
AFISA HABARI MANISPAA.
13.10.2021.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho ameongoza kamati ya siasa CCM Mkoa wa Ruvuma kutembelea na kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea hapo jana tarehe 12 Oktoba 2021 ambayo ilishirikisha wataalamu kutoka Manispaa ya Songea wakiongozwa na Mstahiki Meya Michael Mbano.
Oddo amewataka wataalamu wa Manispaa ya Songea kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kuzingatia matumizi sahihi ya fedha zinazotolewa na Serikali ya Awamu ya sita ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi.
Ametoa rai kwa viongozi na wataalamu kutatua changamoto zote zilizobainika katika kipindi cha utekelezaji wa miradi hiyo. “Oddo alisisitiza”
Miongoni mwa miradi iliyotembelewa ni pamoja na ujenzi wa madarasa 2 na matundu ya vyoo shule ya msingi Ruhuwiko, ujenzi wa maabara ya Sekondari ya Sili, ujenzi wa madarasa 3 shule ya msingi Juhudi, mradi wa bweni Mdandamo Sekondari, ujenzi wa soko la mazao Msamala, ujenzi wa madarasa 2, maabara 1 na matundu ya vyoo Chandarua Sekondari, ujenzi wa bwalo la chakula Sekondari ya Emmanuel Nchimbi.
Mwisho.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa