Kamati ya Siasa Wilaya ya Songea Mjini (CCM) imeridhishwa na utendaji wa kazi wa miradi maendeleo inayoendelea kujengwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea kutokana na miradi hiyo kutekelezwa kwa kiwango kizuri.
Ziara hiyo imefanyika leo 13 Septemba 2022 iliyoongozwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Songea Mjini Hamisi Abdallah Ally ambaye ametembelea miradi mbambali ya maendeleo iliyopo kwenye kata ambapo aliongozana na wajumbe wa kamati ya siasa Wilaya, na Wataalamu kwa lengo la kufanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Miongoni mwa miradi iliyotembelewa ni pamoja na ujenzi wa kituo cha afya Lilambo kilichojengwa kwa shilingi Mil.500 fedha za mapato ya ndani, ujenzi wa shule mpya ya sekondari ya Ruhila iliyopo kata ya Mshangano iliyojengwa kwa shilingi Mil. 470 fedha za mradi wa SEQUIP shule ambayo tayari imefunguliwa rasmi tarehe 05 septemba 2022 na kuanza rasmi msimu wa masomo kwa wananfunzi.
Aidha, walitembelea pia Ujenzi wa kituo cha afya Mletele uliyopo katika kata ya Mletele unaojengwa kwa kwa gharama ya shilingi mil. 545,334,640 fedha kutoka Global fund, ujenzi wa mabweni 4, madarasa 3 kwa shilingi Mil 260 uliyopo shule ya wavulana Songea katika kata ya Seedfarm ukiwa hatua ya kupaua, pamoja na ujenzi wa mabweni 4, na madarasa 3 matatu katika shule ya wasichana Songea kwa gharama ya shilingi Mil. 280 uliopo katika kata ya Mjini.
Hamisi amewapongeza wataalamu wote kwa usimamizi thabiti wa miradi ya maendeleo na amewataka kutatua changamoto ndogondogo zinazojitokeza katika utekeleza miradi hiyo na kukamilisha kwa wakati .
Akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi wa kituo cha Afya Lilambo Afisa Mtendaji wa Kata ya Lilambo Teah Komba alisema bajeti ya mwaka 2021/2022 mradi uliidhinishiwa kiasi cha fedha Mil 500 kutoka mapato ya ndani pamoja na nguvu za wananchi wakiwa wamechangia kiasi cha shilingi 3,295,000 ambapo hadi hivi sasa upo hatua ya ukamilishaji.
Aidha Mkuu wa shule ya Sekondari ya Wavulana Songea Gelasius Lugome alisema mradi huo uliibuliwa na Serikali mwaka 2022 na kutekelezwa kupitia SEQUIP ambao umelenga kunufaisha shule kwa kuongeza madarasa matatu 3 na mabweni 2 mawili kwa lengo la kuongeza udahili wa wanafunzi wa kidato cha tano na kupunguza msongamano mabwenini na madarasani.
Lugome amebainisha kuwa mradi huo unatekelezwa kwa mfumo wa “FORCE ACCOUNT “kama ilivyoamuliwa na Serikali ambapo kwasasa upo hatua ya upauaji kwa mabweni na ujenzi wa madarasa hatua ya ukamilishaji.
Wajumbe wakamati ya siasa wakitoa maoni yao kwa pamoja wameonesha kuridhishwa na mwenendo wa utekelezaji wa miradi yote iliyotembelewa na wamewarai wataalamu kutekeleza miradi hiyo kwa kufauata taratibu za manunuzi zilizowekwa na Serikali.
IMEANDAILIWA NA;
AMINA PILLY
AFISA HABARI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa