Kamati ya Siasa CCM Wilaya ya Songea ikiongozwa na mwenyekiti wa chama hicho Mwinyi Msolomi wamefanya ziara ya kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo na kuridhishwa na utendaji wa kazi wa miradi hiyo.
Ziara hiyo imefanyika leo tarehe 03 Februari ambapo wameweza kufanikiwa kutembelea miradi ya ujenzi wa madarasa 6 katika shule ya Sekondari London kwa shilingi Mil. 120 fedha kutoka Serikali kuu, Ukamilishaji wa vyumba 2 vya madarasa shule ya Msingi Londoni kwa gharama ya shilingi Mil. 25, Upanuzi wa shule za Sekondari kidato cha sita shule ya wasichana Songea kwa shilingi Mil 280.
Aidha Miradi mingine iliyotembelewa ni ukamilishaji wa zahanati ya Makambi kwa shilingi Mil. 50, ujenzi wa vyumba viwili 2 vya madarasa shule ya Sekondari Matogoro kwa shiligi Mil. 40 kutoka Serikali kuu, Ukaguzi wa Barabara Mil. 700 kutoka Tunduru JCT – Seedfarm – Kuchile kwa shilling 398.
Miradi ya upanuzi wa shule za Sekondari ya Wavulana Songea kwa shilingi Mil. 260 pamoja na ujenzi wa kituo cha afya Mletele kwa shilingi 545 fedha za Global Fund, Ujenzi wa chumba 1 cha maabara na cha Kompyuta katika shule ya Sekondari Ruhila na ujenzi wa madarasa 7 bombambili Sekondari kwa shilingi Mil 140 kutoka Serikali kuu ambayo yameanza kutumika.
Msolomi alianza kwa kuwapongeza wataalamu wa Manispaa ya Songea, waheshimiwa Madiwani kwa ushirikiano bora wa usimamiaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo baadhi yake miradi imekamilika na imeanza kutumika na miradi mingine ipo hatua mbalimbali za ukamilishaji. “Alipongeza”
Amewataka wataalamu pamoja na viongozi wa chama ngazi ya Wilaya, kata, Mitaa kuhakikisha wanafuatilia suala la wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza ambao hawajaripoti shule waende shuleni mara moja na amewataka kufanaya vikao shirikishi na wazazi au walezi ili kubaini changamoto zao.
Ametoa wito kwa wazazi na walezi kuhakikisha kila mtoto anapata chakula awapo shuleni ili kujenga afya ya akili ya mwanafunzi ambayo itawezesha kupanda kwa ufaulu wa shule.
Kwa upande wa wajumbe wa kamati ya siasa Wilaya wakitoa maoni kuhusu miradi waliyotembelea ambapo wamewataka wataalamu kumalizia miradi ambayo haijakamilika pamoja na kutekeleza maelekezo yaliyotolewa kuhusu miradi hiyo.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa