KAMATI ya Fedha na Uongozi ya Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Songea Mkoa wa Ruvuma imefanya ziara ya kukagua na kufanya tathmini ya mradi wa Ujenzi wa barabara za mji wa Songea katika kiwango cha lami nzito zenye urefu wa kilometa 8.6.
Jumla ya sh.bilioni 14 zilizotolewa na Benki ya Dunia zinatarajiwa kutumika katika mradi huo. Mradi huo ulianza Juni 2015 na ulitarajiwa kukamilika Juni 30,2017.
Hata hivyo Manispaa ya Songea imevunja mkataba na Kampuni ya Lukolo baada ya muda wake wa Ujenzi kukamilika bila kumaliza kazi.
Kamati ya Fedha na Uongozi imeshauri katika mchakato wa kumpata Mkandarasi mpya, kuhakikisha anapatikana Mkandarasi mwenye sifa na uwezo wa kujenga barabara katika kiwango kinachokubalika na kumaliza kazi ndani ya Mkataba.
Taarifa imetolewa na Albano Midelo
Afisa Habari wa Manispaa ya Songea
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa