• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Songea Municipal Council
Songea Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Songea

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto
      • Planning,Statistics and Monitoring
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu ya Msingi
      • Mazingira na Usafi
      • Maji
      • Afya
      • Elimu ya Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ujenzi
      • Fedha na Biashara
      • Arthi na Mipangomiji
    • Vitengo
      • Uchaguzi
      • Legal Services
      • Mawasiliano, Habari na Teknolojia
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma zetu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi isiyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

KAMISHINA MSAIDIZI WA JESHI LA POLISI MKOANI RUVUMA ACP PILLY MANDE " AKEMEA UNYANYASAJI WA KIJINSIA"

Tarehe ya kuwekwa: March 2nd, 2022

Na;

AMINA PILLY;

AFISA HABARI SONGEA MANISPAA

02 MACHI 2022.

Halmashauri ya Manispaa ya Songea imefanya uzinduzi wa maadhimisho ya Siku ya Mwanamke  Duniani  kuelekea kilele cha  maadhimisho tarehe 08 machi 2022 ambayo hufanyika kila mwaka Duniani kote.

Uzinduzi wa maadhimisho hayo Kihalmashauri ya Manispaa ya Songea yamefanyika  katika viwanja vya bustani ya Manispaa ya Songea  hapo jana tarehe 01 machi 2022 kwa lengo la kuelimisha jamii kuhusiana na usawa wa kijinsia katika nyanja za maendeleo.

Akizungumza katika maadhimisho hayo, mgeni rasmi ambaye alikuwa Kamishina Msaidizi wa jeshi la polisi Mkoa wa Ruvuma ACP Pilly Mande alitoa pongezi kwa wanawake wote wa nchi za Afrika pamoja na kuitaka Serikali kuchukua hatua katika kuhamasisha usawa  katika nyanja za elimu, siasa na uchumi kwa kizazi kilichopo na kijacho ili kuleta maendeleo yenye uwiano sawa kwa wanawake na wanaume.

Mande amewataka wanawake wote nchini kutambua nafasi zao katika jamii kama walimu, wazalishaji, madaktari pamoja na walezi ili  kutengeneza kizazi kinachojali utu na uzalendo  kuanzia katika ngazi ya familia hadi Taifa kwa ujumla.

Amekemea suala la unyanyasaji wa kijinsia katika jamii kwa wanawake ikiwemo na kukosa haki ya kupata elimu, ubakaji pamoja na kupata mimba za utotoni na kutoa wito kwa jamii kuwa walinzi hasa kwa watoto wa kike pamoja na Taasisi za kidini kwa  kuendelea kutoa elimu kwa jamii ili kuondokana na unyanyasaji wa kijinsia.’Alisisitiza’

Kwa upande wake Mratibu wa maadhimisho hayo ambaye pia ni Afisa maendeleo ya jamii Manispaa ya Songea Joyce Mwanja alisema kuwa lengo la maadhimisho hayo ni kutoa fursa ya kuelimisha jamii kuhusiana na jitihada zinazifanywa na Serikali, asasi za kiraia, sekta binafsi na wadau mbalimbali katika kukuza hali ya wanawake wa kitanzania katika nyanja za maendeleo.

Katika utekelezaji wa kutatua changamoto zinazowakabili wanawake kiuchumi, Halmashauri ya Manispaa ya Songea imeendelea kuwawezesha wanawake kwa kutoa mikopo (10%) kila mwaka na katika kipindi cha mwaka 2020/2021 vikundi 1,150 vilipatiwa mikopo yenye jumla ya Tsh. 216,229,441 ambapo vikundi 957 vya wanawake vilipatiwa kiasi cha Tsh. 129,727,777, vikundi 168 vya vijana walipokea Tsh. 64,267,777 pamoja na vikundi 5 vya watu wenye mahitaji maalumu Tsh.22,233,886.”Mwanja alibainisha”

Aliongeza kuwa katika kipindi cha mwaka 2021/2022  Manispaa ya Songea kupitia mfuko wa maendeleo wa wanawake, vijana na watu wenye mahitaji maalumu ilitoa jumla ya Tsh. 465,000,000 ambapo vikundi 5 vya wanawake walipokea Tsh. 310,000,000, vikundi 4 vya vijana Tsh.145,000,000 pamoja na kikundi 1 cha watu wenye mahitaji maalumu Tsh. 10,000,000.

Ametoa rai kwa Serikali kuendelea kutoa mafunzo mbalimbali kwa wanawake ili kuwajengea ufahamu, uwezo na uzoefu ambao utawawezesha katika kurithisha vizazi vyenye haki na usawa katika ngazi zote za maendeleo.

Ikumbukwe kuwa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani  ilianza kuadhimishwa rasmi duniani tarehe 8 Machi 1975 baada ya umoja wa Mataifa kuridhia siku hii kutumika kama siku rasmi kuikumbusha dunia juu ya haki za wanawake.

Kauli mbiu katika Maadhimisho haya mwaka huu ni “KIZAZI CHA USAWA KWA MAENDELEO ENDELEVU”

Mwisho.

 

Matangazo

  • TANGAZO LA LESENI ZA BIASHARA January 22, 2025
  • TANGAZO la usafi wa mazingira Jumamosi ya mwisho wa mwezi Septemba 2024 February 27, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma Yafanikiwa Kurejesha Mil. 9.2, na Kudhibiti Mianya ya Rushwa.

    May 30, 2025
  • TAKUKURU Ruvuma Yawezesha kupatikana fedha za makusanyo Songea Dc

    May 30, 2025
  • ALAT Ruvuma na Baraza la Madiwani la Chalinze Watembelea Manispaa ya Iringa Kujifunza Ukusanyaji wa Mapato.

    May 29, 2025
  • ISMAIL ALI MKIMBIZA MWENGE KITAIFA ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI

    May 15, 2025
  • Tazama zote

Video

ALAT RUVUMA ZIARANI IRINGA TC
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Songea diistrict websites
  • Madaba District Council Website
  • Tunduru District Website
  • Namtumbo District Website
  • Nyasa District Website
  • Mbinga Town Council Website
  • Mbinga District Council Website
  • Songea Municipal face book

Tovuti Mashuhuri

  • Wizara ya Fedha
  • TAMISEMI
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistics
  • Baraza la Mitihani Tanzania

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    SONGEA MUNICIPAL COUNCIL

    Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA

    Simu ya Mezani: 025 2602970

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@songeamc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa