MKURUGENZI WA MANISPAA YA SONGEA ANAWATANGAZIA WANANCHI WOTE KUWA MANISPAA YA SONGE,ITAFANYA KAMPENI YA UPIMAJI WA VIRUSI VYA UKIMWI KATIKA MAENEO YENYE MIKUSANYIKO MIKUBWA YA WATU.KAMPENI HII NI MWENDELEZO WA KAMPENI YA FURAHA YANGU ILIYOZINDULIWA KATIKA MKOA WA RUVUMA TAREHE 30/08/2018.
KAMPENI YA FURAHA YANGU KATIKA MANISPAA YA SONGEA INAANZA TAREHE 15/11/2018 HADI 24/11/208 KAMA RATIBA INAVYOONESHA:
1.TAREHE 15/11/2018,KATA YA MISUFINI,ENEO LA OFISI YA KATA NA SODECO.
2.TAREHE 16/11/2018,KATA YA RUVUMA,ENEO LA STENDI
3.TAREHE 17/11/2018 NA 18/11/2018,KATA YA MJINI,MAENEO YA SOKO KUU NA IKWETA
4.TAREHE 19/11/2018,KATA YA MAJENGO,ENEO LA STENDI YA MALORI
5.TAREHE 20/11/2018,KATA YA MFARANYAKI,ENEO OFISI YA KATA
6.TAREHE 21/11/2018,KATA YA MSAMALA,MAENEO YA STENDI YA MABASI,MTAZAMO NA VETA
7.TAREHE 22/11/2018 NA 23/11/2018,KATA YA LILAMBO,MAENEO YA STANDI NA SINAI
8.TAREHE 24/11/2018 KATA ZA MATOGORO NA LIZABONI,MAENEO YA TTC,VIJIWE VYA BODABODA NA STENDI YA LIZABONI.
HUDUMA HIYO ITATOLEWA KUANZIA SAA 9.30 ALASIRI HADI SAA 2.00 USIKU,LENGO LIKIWA NI KUWAFIKIA WATU WOTE AMBAO MCHANA WANAKUWA NA MAJUKUMU MENGINE YA UJENZI WA TAIFA.
HUDUMA HIYO PIA IMELENGA KUWAFIKIA MAKUNDI MAALUM KATIKA MAENEO YAO YALIOAINISHWA.
WATAKAOGUNDULIKA KUWA NA MAAMBUKIZO YA VVU,WATAPEWA RUFAA YA KWENDA KATIKA KLINIKI ZA TIBA NA MATUNZO ILI WAKAPATE HUDUMA ZAIDI.
WANANCHI WOTE MNASHAURIWA KUJITOKEZA KUPIMA
MIMI NIPO TAYARI KUILINDA FURAHA YANGU,WEWE JE?
TANGAZO LIMETOLEWA NA MKURUGENZI WA MANISPAA YA SONGEA
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa