Kampuni ya Mohamed Gulam Dewji “MO” Enterprise tawi la Songea Mjini imetoa msaada wa chakula kwenye vituo vya kulelea watoto yatima kwa lengo la kuunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya tano, wenye thamani ya shilingi 1,833,000.
Mgeni rasmi katika zoezi hilo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme ambaye aliwakilishwa na Afisa ustawi wa jamii Manispaa ya Songea Vicent Ndumbaro, lililofanyika kwa nyakati tofauti katika vituo vitatu vya kulelea watoto yatima SWACCO iliyopo kata ya Mwengemshindo, ST. ANTON iliyopo kata ya Mfaranyaki, na MCHUNGAJI MWEMA iliyopo kata ya Mjimwema katika Manispaa ya Songea iliyofanyika leo tarehe 05.02. 2021.
Ndumbaro alianza kwa kutoa pongezi kwa kampuni ya Mohammed Enterprise “MO” kwa kutoa msaada wa mafuta ya kula lita 120 yenye thamani ya shilingi 516,000/=, unga wa Sembe kilo 300 wenye thamani ya shilingi 234,000/=, sabuni katoni 12 zenye thamani ya shilingi 120,000/=, sabuni ya unga kilo 90 zenye thamini ya shilingi 168,000/=, Juisi katoni 30 zenye thamani ya shilingi 195,000/=, mbuzi 6 wenye thamani ya shilingi 600,000/=, zenye jumla ya shilingi milioni moja, laki nane, na thelathini na tatu elfu tu 1,833,000/=.
Alibaisha kuwa, Manispaa ya Songea ina jumla ya vituo vya kulelea watoto yatima vitano 5, hivyo bado kuna uhitaji wa wadau/ wahisani mbalimbali kuendelea kujitokeza kwa wingi kusaidia watoto yatima pamoja na wanaoishi katika mazingira hatarishi wanapopta nafasi ya kufanya hivyo.
Naye Angel Issack Samasuba mwakalishi wa Kampuni ya “MO” tawi la Songea Mjini, alisema Kampuni hiyo imekuwa ikitoa msaada mara kwa mara kwa makundi maalmu kwa lengo la kuunga mkono jitihada za Serikali pamoja na kuwapa faraja ili waishi kama jamii nyingine.
Nao walezi wa vituo vya kulelea watoto yatima Kwa nyakati tofauti wakitoa shukarani zao kwenye kampuni hiyo ambapo walisema “ wanaishukuru kampuni ya Mohammed Enterprise kwa msaada uliotolewa kwa watoto hao kwani utawasaidia kupunguza sehemu ya changamoto vituoni mwao na kuwaomba wadau wengine kuwa na tabia ya kuwatembelea watoto yatima vituoni.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
AFISA HABARI MANISPAA YA SONGEA.
05.02.2021
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa