KATA ya Lilambo katika Manispaa ya Songea imeganikiwa kujenga vyumba viwili vya madarasa vilivyogharimu kiasi cha shilingi 1,500,000.
Afisa Mtendaji wa Kata hiyo Agnes Ndunguru amesema kati ya fedha hizo shilingi 10,000,000 ni fedha kutoka Halmashauri ,Shilingi 500,000 ni mchango wa nguvu za Wananchi
Afisa Mtendaji huyo ametoa taarifa ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa shule ya Lilambo B kwa Wajumbe wa Kamati ya siasa Mkoani Ruvuma.
Ndunguru amesema Kata ya Lilambo ni miongoni mwa kata 21 zilizopo katika Manispaa ya Songea ambapo kata hiyo ina jumla ya Mitaa 8 na jumla ya wakazi ni 13956 ,Wanaume 6763 na Wanawake 7193 ,shughuli zinazoendeshwa na wakazi hao ni kilimo ,ufugaji na biashara.
Akiendelea kuzungumza haya amesema mradi wa ujenzi wa Shule ya Msingi Lilambo B uliibuliwa na Wananchi wa Kata hiyo baada ya kukosekana kwa huduma ya Shule katika Mtaa huo ambapo Wananchi walianza kwa kufyatua tofali 72000 na ujenzi ulianza rasmi 06/07/2017 ,matofali yaliyotumika mpaka sasa ni 5400 na tofali 1800 zimesalia.
“Ujenzi umefikia asilimia 85 kazi zilizobaki ni ukamilishaji wa sakafu ,madirisha ,milango ,madawati na ujenzi wa vyoo”.Amesema Ndunguru
Hata hivyo amesema lengo la mradi huu ni kurahisisha upatikanaji wa huduma za Elimu karibu na wakazi wa Mtaa wa Lilambo B wapatao 2041 na lengo la Shule ni kuhudumia wanafunzi 102 ambao wanapata adha kubwa ya kufuata huduma ya Eimu kwa kutembea mpaka Shule iliyopo Mtaa wa Lilambo A.
Eneo limefanyiwa upimaji wa awali na Halmashauri ambapo ukubwa wa eneo ni hekari 4.1.
Imeandaliwa na
Elika Mwakinandi
Wa kitengo cha TEHAMA Manispaa ya Songea
Septemba 3,2019
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa