KATIBU Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Prof.Riziki Shemdoe amesisitiza uwajibikaji wa pamoja katika kikao cha Mkurugenzi wa Elimu TAMISEMI na Wakuu wa shule na Walimu Wakuu mkoani Ruvuma katika kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea Agosti15,2018.
Akizungumza wakati anafungua kikao hicho Profesa Shemdoe amewaagiza Wakuu wa Shule na Walimu Wakuu kuwa washilikishaji katika shughuli zote za kielimu na kutowagawa watu kimakundi.
“Tuwatreat watu equally Iwapo kutakua na ushirikishwaji mzuri wa shughuli zote basi Mkoa wa Ruvuma utafikia hatua nzuri kielimu.” amesisitiza Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma
Ametahadharisha kuwa endapo kutakuwa na makundi katika Ofisi kutasababisha heshima kushuka na pia siri za Ofisi hazitakua siri na hivyo utendaji wa ofisi wenye tija na ufanisi utapungua.
Imetolewa na
Victoria Ndejembi,
Kitengo TEHAMA Manispaa Songea,
16,Agosti 2018.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa