Katibu Tawala Wilaya ya Songea Mtella Mwampamba amewataka Maafisa Watendaji wa kata kushirikiana na kamati za lishe za kata kuendelea kutoa elimu kwa wazazi namna ya uandaaji wa lishe kwa watoto chini ya miaka mitano pamoja na wamama wajawazito ili kuepuka utapiamlo na udumavu.
Agizo hilo limetolewa tarehe 19 Oktoba 2023 katika kikao cha utekelezaji wa lishe kilichofanyika katika Ukumbi wa Manispaa ya Songea na kuhudhuriwa na Maafisa Watendaji Kata 21 kwa lengo la kufanya tathimini ya utekelezaji wa Mkataba wa Lishe katika kipindi cha robo ya mwaka Julai – Septemba, 2023.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa