Mstahiki Meya Manispaa ya Songea Michael Mbano, ameishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuleta fedha zaidi ya Bil. 188 kwa ajili ya kuboresha huduma na miundombinu mbalimbali ya miradi ya maendeleo.
Katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wake Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Sekta ya Elimu Msingi na Sekondari Halmashauri ya Manispaa ya Songea imefanikiwa kujenga jumla ya madarasa 244 yenye thamani ya 5,234,000,000 inayojumuisha viti, meza na madawati.
Sambamba na miradi hiyo Halmashauri imepokea fedha kiasi cha bil. 3,600,000,000 ambazo zimewezesha ujenzi wa shule mpya (4) za Sekondari ikiwemo na shule ya sekondari ya Dr. Lawrance Gama, Luhira Sekondari, Dr. Damas Ndumbaro, pamoja na shule maalumu ya Amali Ruvuma.
Alisema Halmashauri imefanikiwa kujenga shule maalumu ya awali na Msingi ya mchepuo wa lugha ya kiingereza ambayo imejengwa kwa shilingi mil. 800 fedha za mapato ya ndani ambayo katika ziara yake Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan iliyofanyika tarehe 24/09/2024 aliifungua shule hiyo ambayo ina jumla ya wanafunzi 491 kwa wanafunzi wa Msingi na Awali.
Elimu bure Manispaa ya Songea inapokea kila mwezi jumla ya kiasi cha shilingi 298,000,000 ikiwa shule za Sekondari kiasi cha shilingi 231,000,000 na shule za Msingi shilingi 67,000,000 ambapo katika kipindi hiki sekta ya elimu Halmashauri imepokea jumla ya bil.14.24.
Alisema taratibu za kujenga Chuo Kikuu cha uhasibu katika eneo la Pambazuko Manispaa ya Songea zimekamilika na muda wowote ujenzi wa chuo hicho utaanza ambapo kiasi cha Bil 17.8 kwa ajili ya utekelezaji wa kazi hiyo kimetolewa, pia kuhusu fidia za maeneo hayo tayari wameshalipwa na kufikia jumla ya fedha zilizotolewa sekta hiyo ni shilingi i Bil. 41.78
Mhe. Mbano alibainisha kuwa, katika Sekta ya afya Manispaa ya Songea imepokea jumla ya Bil 6,735,143,347 ambapo kati ya fedha hizo shilingi bil. 5 zimepelekwa kwenye ujenzi wa Hospitali ya Manispaa ya Songea 1, Ujenzi wa Vituo vya afya 4, pamoja na Zahanati 4 ambapo kiasi cha shilingi Bil. 1.735 ni fedha za matibabu ikiwa ni wastani shilingi 40,744,000 kila mwezi ambapo hapo awali ilikuwa shilingi Mil. 18,000,000 pekee.
Aliongeza kuwa, katika kikindi cha miaka (4) hali ya utoaji wa huduma ya maji imeimarika kutokea asilimia 82 hadi asilimia 92 katika Manispaa ya Songea, Nanukuu “Tunamshukuru Mheshimiwa Rais kwa mradi wa maji wa Bil 145.7 wa miji 28 katika Manispaa ya Songea ambapo mradi huo ukikamilika hali ya upatikanaji wa maji Manispaa ya Songea utakuwa asilimia 100.” Mwisho wa kunukuu.
Sekta ya miundombinu ya barabara Manispaa ya Songea imepokea kiasi cha Bil. 22 kwa ajili ya ujenzi wa barabara (TACTIC) za lami nzito katika kata za mjini yenye urefu wa KM 10.1 ambapo utekelezaji wake umefikia 89%. pia Halmashauri imekamilisha ujenzi wa Standi ya kuu ya Mabasi Songea kwa kiasi cha Bil. 6.5.
Aidha, Mafanikio katika Sekta ya huduma za jamii ( TASAF), Manispaa ya Songea jumla ya Bil.9 zimepokelewa na kulipwa kwa wafaidika 2514.
Mbano alisema asilimia 60 ya wakazi wa Manispaa ya Songea wamefaidika na ruzuku ya mbolea hivyo imewezesha kuimarisha uchumi wa kaya na wa Taifa ambapo katika kipindi cha miaka minne TAN 88,208 zimetolewa ruzuku kwa wananchi wa Manispaa ya Songea.
Akizungumzia kuhusu mikopo ya makundi maalumu wanawake 4%, vijana 4% na watu wenye ulemavu 2% katika kipindi cha miaka (4) Manispaa ya Songea imetoa jumla ya bil. 2,205,429,441 .
Aliongeza kuwa, “hivi karibuni Halmashauri imepata kibali cha kutoa mikopo kupitia benki ya NMB ambapo jumla ya Bil. 1.3 zipo katika hatua ya kukopeshwa pia Halmashauri imefanikiwa kulipa fidia ya jumla ya 5,300,000,000 kwa eneo la EPZA kata ya Mwenge Mshindo na shilingi 900,000,000 Bonde la Ruhira.” Alibainisha.
Ukusanyaji wa mapato ya ndani yameongezeka kutoka shilingi Bil. 2.1 hadi shilingi bil. 6.8 ambapo bajeti ijayo 2025/2026 Halmashauri inatarajia kukusanya jumla ya shilingi Bil. 9.
Hayo yamejiri tarehe 21 Machi 2025 wakati akizungumza na waandishi wa Habari iliyofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Songea kwa lengo la kuelezea mafanikio ya miaka 4 minne chini ya uongozi wake Dkt. Samia Suluhu Hasssan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa ujumla, Meya Michael Mbano alieleza kuwa miradi mbalimbali ya maendeleo inayoendeshwa kwa ushirikiano wa serikali na wananchi inaimarisha uchumi wa kaya na taifa kwa ujumla, na kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake katika kuboresha huduma na miundombinu katika Manispaa ya Songea.
MWISHO.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa