Afisa elimu TALGWU Taifa ndugu Beda Kihindo amewataka watumishi wanachama wa cha Serikali za Mitaa Tanzania TAGWU Mkoa wa Ruvuma kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kudumisha ushirikiano mahala pa kazi ili kufanya kwa ufanisi.
Kihindo aliongeza kuwa Serikali imeboresha huduma kwani inatoa stahiki za watumishi bila kujali jinsi wala upendeleo ambapo alisema tukiondoa watumishi wasio waalimu katika utumishi asilimia 60 walioajiriwa ni wanawake, hivyo alitoa rai kwa wanawake hao kutenga muda wa kazi na kwenda kushiriki masomo ili kuweza kujiendeleza kielimu.
Kauli hiyo imetolewa siku ya kilele cha maadhimisho ya mwanamke duniani ambayo ilifanyika tafrija ya usiku wa mwanamke duniani iliyofanyika katika ukumbi wa Angrican kwa lengo la kutoa elimu ya chama, na kuzungumza na wanawake wa chama hico.
Imeandaliwa na;
Amin a Pilly
Kitengo cha mawasiliano Serikalini.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa