Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha Taifa Dkt. Frank Hawas amewapongeza viongozi wa CCM Wilaya ya Songea Mjini baada ya kutembelea miradi ya chama inayotekelezwa na chama hicho ambapo ametoa wito kwa wananchama, viongozi na wadau kuendelea kuchangia michango katika kuendeleza ujezi wa ofisi za chama za kata.
Dkt. Hawas ametoa pongezi hizo akiwa Mkoani Ruvuma alipotembelea miradi Songea Mjini tarehe 09 Novemba 2023 ambapo alifanikiwa kutembelea ujenzi wa ofisi ya chama kata ya Msamala, Kata ya Mshangano, pamoja na miradi inayosimamiwa na umoja wa Wazazi Mkoani Ruvuma.
IMEANDALIWA
AMINA PILLY
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa