Katibu Tawala Wilaya ya Songea Mtela Mwampamba, amewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa wataalamu wa afya katika zoezi la linaloendelea la umezeshwaji wa dawa za kinga tiba ya Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ikiwemo na Usubi, na Minyoo ya tumbo ambalo limeanza kufanyika leo tarehe 17 hadi 21 August 2024.
Zoezi hilo hufanyika kila mwaka Kitaifa chini ya Wizara ya Afya kwa kushirikiana na RTI, ambapo kwa Manispaa ya Songea zoezi hilo limeanza kufanyika leo tarehe 17 hadi 21 Agosti 2024, ambayo itafanyika kwa kata zote 21 na Mitaa 95 kwa walengwa wenye umri wa miaka 5 na kuendelea.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo tarehe 17 Agosti 2024, amewataka wananchi hao kushiriki kikamilifu katika zoezi la umezeshwaji wa dawa za usubi na minyoo ambalo linasimamiwa na wataalamu wa afya pamoja na wahudumu waliopewa mafunzo maalumu ya ugawaji wa dawa kutoka kila mtaa ambao watapita kwenye kaya 76,843 zilizopo ndani ya Manispaa ya Songea.
Kwa upande wake Mratibu wa Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Bload Komba alisema “ kabla ya kuanza zoezi hilo, wamewza kutoa mafunzo kwa wataalamu wa afya sambamba na kuendelea uktoa wa elimu kwa wananchi kupitia wenyeviti wa mitaa 95.
Alisema lengo la zoezi hilo ni umezeshaji wa kinga tiba kwa jamii kwa lengo la kuwafikia asilimia 80% kwa wananchi wasiopungua 250,000 kati ya 306,134, kwa kaya 76,843.
Miongoni mwa dalili za ugonjwa wa usubi ni pamoja na ngozi kuwasha sana, ngozi kuwa na ukurutu usiotibika, ngozi kuchakaa mithili ya ngozi ya kenge au mamba, ngozi kuwa na mabaka mabaka mithili ya mtu aliyeungua na moto kama ya chui.
Bload alibainisha Madhara ya magonjwa yake ni pamoja na kutokuona vizuri na hatimaye upofu, kushindwa kufanya kazi nan a hivyo kuwa tegemezi na umaskini katika kaya na jamii.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa