HALMASHAURI ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma imekuwa ikitekeleza shughuli za Mfuko wa wa Afya ya jamii (CHF) tangu mwaka 2006 ambapo hadi kufikia Machi 2018, kaya 7045 sawa na asilimia 11 ya kaya zote za Manispaa 60,036 zilikuwa zimejiunga na CHF.
Pia utoaji wa vitambulisho bure kwa wazee wenye umri wa kuanzia miaka 60 umefanyika kwa wazee 1,200 sawa na asilimia 10.9 lengo likiwa ni kuwafikia wazee 11,678 katika Kata zote 21.
Katika kutekeleza mpango huo,Halmashauri ya Manispaa ya Songea, imeingia mkataba na vituo vya kutolea huduma za afya ambavyo vinamilikiwa na Mashirika ya dini kutoa mitibabu bure kwa wazee 600.
Hata hivyo Halmashauri ya Manispaa ya Songea imekuwa ikipokea dawa na vifaa tiba toka serikali kuu kwa asilimia 91.1 hadi sasa,ambapo Halmashauri hununua dawa za nyongeza kufidia zile zinazokosekana Bohari ya dawa MSD kupitia vyanzo vingine vya fedha ikiwemo Mfuko wa pamoja wa afya, Bima ya Afya, CHF na fedha za papo kwa papo.
Magonjwa yanayoongoza katika Manispaa ni Malaria kwa asilimia 34,magonjwa ya mfumo wa hewa asilimia 32.3,magonjwa ya njia ya mkojo(UTI) asilimia 11.2,Magonjwa ya ngozi asilimia 9.9,Magonjwa ya vichomi(Nimonia) asilimia 7.6 na magonjwa ya kuhara kwa asilimia tano.
Halmashauri ya Manispaa ya Songea ina jumla ya vituo vya kutolea huduma za afya 35, ambavyo kati ya hivyo Hospitali ni moja Vituo vya Afya ni vitatu, na Zahanati ni 31.
Imeandikwa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
Septemba 11,2018
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa