KIKUNDI cha Bariki ni miongoni mwa vikundi vinavyojishughulisha na ufugaji wa ng’ombe wa maziwa katika Manispaa ya Songea. Kikundi hiki kilichopo Kata ya Lilambo kilianzishwa mwaka 2013 kwa usajili namba CBO/00409 wa tarehe 21-08 –2013 Kikiwa na idadi ya wanachama 18 ambapo wanawake ni 17 na mwanaume ni mmoja.
Lengo la mradi ni kuboresha lishe, kutoa ajira kwa vijana, kuongeza kipato cha wanakikundi na hatimaye kuinua uchumi wa viwanda kwa kuanzisha kiwanda kidogo cha kusindika maziwa.
Taarifa za kikundi hicho inaonesha kuwa kikundi hiki kilipatiwa mradi wa Ng’ombe wanane kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Songea Aprili 2017. Kwa sasa idadi ya Ng’ombe imeongezeka kutoka ng’ombe wanane hadi 12, hii ni kutokana na kuzaliwa ndama wanne. Mradi huu mpaka sasa umegharimu zaidi ya shilingi milioni 12.
Uzalishaji wa maziwa ni wastani wa lita 13 mpaka 15 kwa siku kwa kila ng’ombe. Endapo ng’ombe wote watazaa, uzalishaji wa maziwa kwa miezi 10 kwa ng’ombe wote 8 zitapatikana lita 36,400 na kukipatia kikundi Shilingi 30,940,000.00 kwa wastani wa bei shilingi 700 mpaka 1000. Fedha hizi zitatusaidia kusomesha watoto,kuchangia bima za afya na kujenga nyumba za kisasa.
Malengo ya baadaye ya kikundi ni kuanzisha kiwanda kidogo cha usindikaji maziwa kwa sababu ndani ya kata ya Lilambo kuna jumla ya ng’ombe 882 wa asili na wa kisasa wanaozalisha maziwa lita 77520 kwa mwaka.
Ni matarajio kwamba mradi huu utawakwamua wanakikundi na umaskini na kuwafikisha kwenye uchumi wa viwanda endapo soko la maziwa litaboreka
Imetolewa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
Juni 10,2018.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa