kisiwa cha Mbambabay wengine wanakiita kisiwa cha Zambia kilichopo Mbambabay wilayani Nyasa mkoani Ruvuma ambacho kimependekezwa kuwa Hifadhi ya wanyamapori.Kisiwa hicho kina ukubwa wa hekta 27.kisiwa hicho kimejaliwa kuwa na uoto unaovutia wa misitu ya miombo ambao ni maarufu duniani ambapo mawe yanayozunguka katika kisiwa hicho ni mazalia ya samaki wa mapambano aina zaidi ya 400 wanaopatikana katika ziwa Nyasa pekee.
Kutokana na udogo wa kisiwa cha Mbambabay Afisa Maliasili na Utalii wa Mkoa wa Ruvuma Afrikanus Challe anashauri katika kisiwa hicho kusijengwe makazi ya kudumu kwa ajili ya wafanyakazi wa kuhudumia watalii ili kuendelea kutunza uoto wa asili uliopo hivi sasa
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa