MAMLAKA za Serikali za Mitaa ndizo zilizopewa Majukumu na Mamlaka ya kukusanya mapato ya ada na ushuru mbalimbali kwa kutumia sheria mama yaani zilizotungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na sheria ndogo zinazotungwa na Halmashauri.
Hivyo Halmashauri ina jukumu la kuweka mazingira wezeshi ya kufanya shughuli za biashara na mikakakati mbalimbali kwa ajili ya kukusanya Mapato kutoka vyanzo vilivyoidhinishwa na serikali na vilivyobuniwa na Halmashauri vinakusanywa na kuhakikisha kila chanzo kilichobuniwa kinafikia malengo/makisio yanayopangwa kila mwaka.
Lengo la Serikali kuzipa Mamlaka serikali za Mitaa ni Kuboresha na kuongeza wigo wa Mapato ya ndani ya Halmashauri kwa ajili ya kuimarisha utoaji wa huduma bora za Msingi kwa wananchi na kuwa na uwezo wa kiuchumi na kumudu uendeshaji wa shughuli za halmashauri za kila siku.
Halmashauri ya Manispaa ya Songea ina jumla ya wafanyabiashara 10,486 ikiwa wafanyabiashara 3034 ni wafanyabiashara walio rasimishwa kwa kupewa Leseni za Biashara. Kati ya hao wafanyabiashara 2,748 ni wa aina mbalimbali za Biashara 286 ni wafanyabiashara wa Bar na Grocery, 203 ni nyumba za kulala wageni, 1,820 ni wafanyabiashara wadogo walioko kwenye masoko ya manispaa na kwa upande wa pikipiki za magurudumu mawili na Matatu inakadiriwa kuwa kuna jumla ya pikipiki 4,000 zinazosafirisha abiria katika Manispaa ya songea
Aidha Manispaa ya Songea inawafanyabiashara wasio rasmi wapatao 2,080 ambao wanaendesha shughuli zao katika maeneo yasiyo rasmi ambayo hayajatengwa na halmashauri kwa ajili ya shughuli za biashara.
2.0 SHERIA ZINAZOSIMAMIA SHUGHULI ZA BIASHARA
Katika kuhakikisha shughuli za Biashara na Viwanda zinaendeshwa kwa kufuata taratibu na sheria, Serikali imeweka sheria mbalimbali kwa ajili ya kusimamia uendeshaji ya shughuli za biashara. Sheria hizo ni kama ifuatavyo:
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa