Mkuu wa Wilaya ya Songea amewataka wananchi kumia nishati mbadala kwa ajili ya kupikia na kuondokana na matumizi ya kuni ambapo hupelekea kutokea kwa jangwa na kupoteza uoto wa asili.
Kauli hiyo imeshauriwa leo kwenye kikao cha kamati ya ushauri ya Wilaya ya Songea DCC ambacho kimefanyika tarehe 24 januari 2025 katika ukumbi wa HOMSO Songea ambacho kimehudhuriwa na wadau mbalimbali kwa lengo la kufanya ufuatiliaji na tathimini ya utendaji wa kazi na maagizo yaliyotewa kikao kilichopita kupitia Halmashauri 3 ambazo ni Madaba, Songea na Manispaa ya Songea.
Miongoni mwa mikakati iliyopangwa ili kujenga maendeleo katika sekta mbalimbali wilayani humo ni pamoja na kutoa elimu kwa jamii namna ya matumizi sahihi ya nishati mbadala ambayo ni makaa ya mawe, kuandaa mkakati wa kudhibiti utoro kwa shule za Sekondari na Msingi, udhibiti wa ufugaji holela wa ng'ombe, na mengineyo.
Akizungumza Afisa misitu Manispaa ya Songea na Betram Njelekera alisema, katika kuunga mkono jitihadaza Serikali ya awamu ya sita katika kudhibiti uharibifu wa mazingira kupitia Mbungea wa jimbo la Songea mjini amewezesha vikundi 12 ambapo waliwezesha kugawa mitungi ya gesi 84 kwa mama lishe ili jamii iondokane na uharibifu wa mazingira.
Kikao hicho hufanyika mara moja kila mwaka ili kufanya mapitio ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Serikali kupita Wilaya ya Songea.
IMEANDALIWA;
AMINA PILLY
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa