Naibu Meya Manispaa ya Songea Jeremiah Milembe ameongoza kikao kazi cha baraza la Madiwani kilichofanyika leo tarehe 14 Feruari 2023 katika ukumbi wa Manispaa ya Songea kilichohudhuriwa na wakuu wa Idara na vitengo, Watendaji wa kata, kwa lengo la kupokea taarifa na kuzijadili ili kutatua changamoto mbalimbali zinazozikabili kata kuelekea Mkutano wa Baraza la Madiwani litakalofanyika tarehe 16 Februari 2023.
Waheshimiwa Madiwani kwa nyakati tofauti wametoa maoni yao kupitia kikao hicho ambapo wameipongeza Halmashauri kuweka utaratibu wa kuanza kikao cha kazi kwanza kabla ya Mkutano wa Baraza la Madiwani ambao husomwa na kujadili taarifa mbalimbali za kamati kudumu za Halmashauri.
Aidha kupitia kikao hicho zimejadiliwa changamoto mbalimbali za kwenye kata na kutolewa majibu ya papo kwa papo kutoka kwa wataalamu.
Imeandaliwa;
Amina Pilly;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa