Mpango wa Elimu ni muongozo wa Elimu ambao ulianza mwaka 2023 na kuzinduliwa na Waziri Mkuu tarehe 04.08.2024 Mkoani Tabora kwa lengo la kuboresha utekelezaji wa Mpango wa elimu.
Katika kutekeleza mpango huo ilifanyika tathimini na kubaini kuwepo kwa baadhi ya mapungufu mbalimbali ambayo ililazimika kuboresha utendaji wa kazi wa mpango wa elimu (KPI).
Tukio hilo limefanyika tarehe 01 Juni 2024 katika uwanja wa shule ya Wavulana Songea kilichofanyika kwa lengo la kuwakumbusha walimu hao misingi na majukumu ya kazi yao ambacho walihudhuria wakuu wa shule za Msingi na Sekondari, Maafisa wa elimu, pamoja na walimu wote wa Manispaa ya Songea.
Akizungumza mwakilishi wa Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI (ELIMU) Vicent Boniface Kayombo amewataka walimu hao kuendelea kusimamia malezi ya watoto bila kukata tama ili watoto waweze kujengeka kimaadili na kuwa ufaulu mzuri.
Alisema ili malezi ya watoto yaweze kukamilika inahitaji ushirikiano wa walimu, mahusiano na mawasiliano bora baina ya Mkuu wa shule na Walimu pamoja kufundisha na kufaulisha wanafunzi na kuondoa zero 0 kwa wanafunzi.
Amewataka kuzingatia mambo makuu mnne kwa wanafunzi ikiwemo umri wa watot, utayari wa mtoto, Mazingira ya mtoto pamoja uwezo wa mtoto pia ametoa wito kwa walimu wa shule za Sekondari kutumia lugha ya kiingereza kwa kipindi chote cha masomo isipokuwa somo la Kiswahili.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa