MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amefungua kikao cha wadau cha kutambua viashiria na Changamoto zinazoukabili ushoroba wa Selous-Niassa.Hotuba ya Mkuu wa mkoa wa Ruvuma imesomwa kwa niaba yake na Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Sophia Kizigo.Jukwaa hilo linalofanyika kwa siku mbili kwenye ukumbi wa chuo cha VETA Songea linafadhiliwa na WWF.Utafiti uliofanywa mwaka 2009 unaonesha kuwa iwapo hatua za kuulinda ushoroba wa Selous-Niassa hazitachukuliwa,kuna hatari ushoroba huo kutoweka baada ya miaka 20 ambapo hivi sasa tayari miaka kumi imefika.HATIMAYE limeundwa Jukwaa la Maendeleo na uimarishaji wa ulinzi na uhifadhi wa Ushoroba wa Selous-Niassa baada ya kukamilika kwa warsha ya wadau wa uhifadhi kilichoratibiwa na WWF kwa siku mbili kwenye ukumbi wa VETA mjini Songea.Jukwaa Hilo litakuwa linakutana kila baada ya miezi sita ili kukabiliana na Changamoto za ushoroba wa Selous-Niassa ili kuhakikisha ushoroba huo unakuwa endelevu kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa