Kikundi cha Tumaini kata ya Lilambo Manispaa ya Songea kimetoa shukrani za dhati kwa Serikali ya awamu ya sita kwa kuwakopesha fedha kiasi cha shilingi milioni 70 ambazo zimetumika katika ujenzi wa jengo la uwekezaji na kununua mashine mil. 36,300,000 itakayotumika kwa ajili ya kukamua alizeti.
Afisa Maendeleo ya jamii Manispaa ya Songea Martin Mtani alisema “Manispaa ya Songea imetenga maeneo rasmi ya uwekezaji wa viwanda kwa vikundi 11 vya ushonaji, kiwanda cha utengenezaji wa batiki, kiwanda cha uchakataji maziwa, kiwanda cha Welding na Aluminium, kiwanda cha uchakataji wa mazao ya nyuki pamoja na kiwanda cha uchakataji wa mafuta ya alizeti.”
Mtani aliongeza kuwa kupitia Idara ya Maendeleo ya jamii imeendelea kusimamia utoaji wa mikopo ya asilimia 10% kwa wanawake 4%, vijana 4% na walemavu 2% kwa mwaka 2021/2022 Tshs milioni 465 zilitolewa kwa vikundi ambapo katika mkakati waliojiwekea wanakikundi hao nikuhakikisha wanalima hekari za kutosha za zao la alizeti ili kuwa na malighafi za kutosha.
Alisema mikopo iliyotolewa ni kwa ajili ya uwekezaji pamoja na shughuli za kiuchumi ambapo kupitia mikopo hiyo kikundi cha Tumaini ambacho hujishughulisha na ukamuaji wa mafuta ya alizeti wameweza kununua mashine ya kukamua alizeti na karanga kwa gharama ya shilingi mil. 36,300,000 ambayo tayari imefungwa na imeshaanza kufanya kazi ya kukamua alizeti. “Alibainisha.”
Kwa upende wake Mhandisi Fredrick Mbawala amesema amepokea mashine ya kikundi cha Tumaini ambapo tayari ameifunga na imeshaanza kufanya kazi ambapo alisema mashine hiyo inauwezo wa kupepeta alizeti na kutenganisha mawe au takataka na alizeti, pia inakamua mafuta, inachemsha, na kuchuja.
Amewataka wananchi na wadau kuleta mazao yao ya alizeti katika kiwanda hicho ili waweze kukamua mafuta, kuununua mafuta, mashudu na huduma nyinginezo.
AMINA PILLY
KITENGO CHA MWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa