MKUU wa Wilaya ya Songea Mheshimiwa Kapenjama Ndile amewataka wananchi kutoamini zao la kiuchumi kuwa ni zao la Mahindi pekee bali wafahamu kuwa kuna mazao mbadala ambayo yanaweza kuwainua kiuchumi ikiwemo na zao la ufuta, na mazao mengine.
Alisema kwa mwaka 2024 Kimkoa wameuza ufuta wenye thamani ya kiasi cha tani Bil 20 kiwilaya Mil 20 ambayo ni zaidi ya kilo 700 ambapo zao hilo linasoko kubwa katika nchi ya China, Irani na Uturuki.
Kauli hiyo imetolewa tarehe 02 Desemba 2024 wakati akizungumza na wakulima wa kata ya lilambo kwa lengo la kuhamasisha wakulima kulima zao la biashara nje ya zao la mahindi ili kuboresha kipato cha mkulima.
Akizungumza Afisa Kilimo Manispaa ya Songea Zawadi Nguaro alisema Manispaa ya Songea imepokea kilo 500 sawa na tani 0.5 za ufuta kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ikiwa ni makato ya mauzo ya ufuta ya shilingi 25 kutoka kwa wakulima ambapo wakulima 77 wenye mashamba 143 watanufaika mbegu bila malipo yoyote.
Wakizungumza wakulima hao wameishukuru Serikali kwa kuwapatia mbegu hizo za ufuta ambapo wameahidi kulima kwa kufuata utaratibu wa kilimo bora.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa