Wananchi wa kata ya Lilambo Manispaa ya Songea wametoa shukrani kwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kujenga kituo cha Afya ambacho kimejengwa kwa gharama ya shilingi Mil.500 fedha zilizotokana na Makusanyo ya mapato ya ndani.
Hapo awali wananchi wa kata ya Lilambo walikuwa wanapata huduma za afya katika Zahanati na walipohitaji kupata huduma kubwa za matibabu walilazimika kutembea kwa umbali mrefu au kukodi usafiri kwa gharama kubwa kuelekea Hospitali kubwa jambo ambalo lilikuwa kero kwa wananchi lakini baada ya kujengwa kituo na kuanza kutoa huduma za awali kituoni hapo, wananchi wameondolewa adha zilizojitokeza hapo awali. “ Wananchi wameshukuru”
Hayo yamejili jana tarehe 02 Januari 2023 katika uzinduzi wa utaoaji wa huduma za awali za matibabu katika kituo cha afya Lilambo kwa lengo la kuondoa kero na kusongeza huduma kwa wananchi.
Mkuu wa Idara ya Mipango na Uratibu Manispaa ya Songea Andambike Kyomo alisema “Ukamilishaji wa kituo hicho umetumia miongozo ya Wizara ya Afya TAMISEMI pia ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi wa Chama Cha Mapinduzi CCM ambayo imeelekeza kutatua kero za wananchi na kusogeza huduma bora kwa jamii.” Alisisitiza”
Kyomo aliongeza kuwa Kituo hicho kimejengwa kwa gharama ya shilingi Mil. 500 fedha kutoka mapato ya ndani pia ni utekelezaji wa maelekezo ya Mheshimiwa Waziri Mkuu kuwa kila Halmashauri ijenge kituo cha afya kupitia mapato yao ya ndani ya Halmashauri.
Mafanikio hayo yametokana na ushirikiano wa karibu na viongozi ngazi ya Mkoa, Wilaya, Mbunge, Wakuu wa Idara na Vitengo, Watendaji wa kata na Mitaa, Waheshimiwa Madiwani na wananchi kwa ujumla na kufikia hatua ya kukamilisha ujenzi na kuanza kutoa huduma za awali za matibabu kwa wananchi. Kyomo alishukuru."
Kwa upande wake Mheshimiwa Diwani kata ya Lilambo Yobo Mapunda alianza kwa kutoa shukrani kwa uongozi na wananchi kwa kufanikiwa kujenga kituo cha afya na kuanza kutoa huduma za awali kwa wananchi ambapo itawasaidia wananchi kuwa punguzia adha ya kutembea mwendo mrefu kufuata matibabu . “alishukuru”
Yobo alibainisha kuwa kituo cha afya Lilambo tayari tumepokea waganga wawili 2 na wahudumu wa afya watatu 3 kwa ajili ya kuanza kutoa huduma za kitabibu ambapo kwasasa huduma zitakazotolewa ni huduma za awali na baada ya kukamilika kwa miundombinu na vitendea kazi huduma nyingine zitatolewa.
Naye kaimu mganga Mkuu Manispaa ya Songea Beda Mgegedu alisema aina ya matibabu yatakayoanza kutolewa katika kituo hicho ni huduma za awali (OPD na maababra na baada ya kukamilika kwa taratibu nyingine huduma kubwa za matibabu zitatolewa.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa