MKUU wa Wilaya ya Songea Pololet Mgema amesema mradi wa kituo cha afya Kata ya Ruvuma Manispaa ya Songea ambao serikali ilitoa shilingi milioni 400, kinatarajia kufunguliwa na mbio za Mwenge wa Uhuru Septemba 22,2019.
Akizungumza mara baada ya kukagua mradi huo akiwa ameongozana na Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Songea ,amesema kwa ujumla mradi umekamilika kwa zaidi ya asilimia 99 ambapo hivi sasa imebaki kufungwa milango ili kiweze kuanza kazi ya kuwahudumia wananchi.
Mgema amesema ufunguzi wa kituo hicho ukifanyika ,serikali italeta watumishi,madawa na vifaa tiba ili kusogeza huduma kwa wananchi wa Manispaa ya Songea.Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Dkt.Mameritha Basike amesema kituo hicho kinatarajia kuhudumia wakazi zaidi ya 45,000 wa Manispaa ya Songea kutoka kata za Subira,Majengo na Mateka.
Amesema majengo yote manne yamekamilika ambayo mi wodi ya wagonjwa wa nje,wodi ya upasuaji,mama na mtoto na jengo la maabara.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa