Mstahiki Meya Manispaa ya Songea Alhaji Abdul Hassani Mshaweji, amesema “Maendeleo ya Nchi hayawezi kuja bila uwekezaji”.
Kauli hiyo imetolewa katika kikao cha Wadau wamiliki wa Vyombo vya usafirishaji abiria,Viongozi wa Wasafirishaji abiria Mkoa wa Ruvuma(UWARU), pamoja na wadau wa usafirishaji ambao ni (RTO), LATRA, TARURA, Kilichofanyika tarehe 02/03/2020 katika ukumbi wa Manispaa ya Songea.
Mshaweji alisema Ujenzi wa Stendi ya shule ya Tanga umekamilika na sasa iko tayari kwa ajili ya kuanza kutoa huduma ikiwa pamoja na Halmashauri kuanza kukusanya mapato kupitia Stendi hiyo. Alisema Stendi hiyo ina jumla ya Vibanda 50, ikiwa Vibanda 30 ni Vibanda kwa ajili ya shughuli za biashara na Vibanda 20 ni kwajili ya kukatia tiketi za mabasi.
Alisema, “ makubaliano yaliyofanyika na wadau wote kwa stendi zote (4) ni pamoja Mabasi yaendayo Dar es salaam, Njombe, Iringa, Mbeya, Sumbawanga, Dodoma,kupitia barabara ya Njombe safari zao zitaanzia Stendi ya Tanga na zinaporejea safari zake zitaishia stendi kuu ya Tanga.
Mabasi yaendayo kupitia barabara ya Lindi kwenda Dar es salaam, Lindi, Mtwara, Tunduru yataanzia Stendi ya Tanga kupitia Stendi ya Msamala na Seedfarm, na yanaporejea yatapitia Stendi ya Seedfarm kuishia stendi ya Msamala.
Mabasi yanayoelekea njia ya Mbinga, Nyasa, na Songea vijijini safari zake zitaanza Stendi ya Msamala kupitia stendi Mfaranyaki kwa dakika 10 tu, na yanaporejea yatapitia Mfaranyaki na kuishia safari zake stendi ya Msamala. Pia daladala zote za Mshangano, Tanga, Mlilayoyo zitaanza safari stendi ya Mfaranyaki kupitia Msamala, Tanga na kuelekea zinakomalizia safari zake.
Aidha, Mabasi yaendayo Makambako na Njombe yatapitia stendi kuu Tanga na kumalizia safari zake Stendi Msamala. Pia Mabasi yanayotokea barabara Lindi yaendayo Mbeya , Njombe na Iringa yataruhusiwa kuingia katikati ya Mji kama yatakuwa na Abiria au kujaza Mafuta.
Aliongeza kuwa magari yanayotoka maeneo ya Matimila,Mletele, Ngwinde, na Chengena safari zao zitaanzia kituo cha Daladala cha Majengo- -Mitumbani na kumalizia safari zake katika kituo hicho. Pia Magari yaendayo Mpitimbi ,Mkenda, Muhukuru, Namatuhi, Ndongosi na Namabengo zitaanzia kituo cha daladala majengo—mitumbani na kumalizia kituo hicho.
Naye Mratibu wa Polisi Mkoa wa Ruvuma SP Salumu Morimori aliseama” kazi ya Jeshi la polisi ni kusimamia Sheria na Taratibu zilizowekwa na Serikali, hivyo aliwaasa wamiliki wa Vyombo vya Moto na Madereva kufuata makubaliano haya ambayo mmeyapitisha na atakaye kwenda kinyume na makubaliano haya atachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo na kupelekwa mahakamani.”Alisisitiza.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY
KAIMU AFISA HABARI MANISPAA YA SONGEA.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa