Magonjwa ya figo huchelewa kuonesha dalili zake, wahi mapema kupima ili uijue afya yako.“afya yako ndiyo mtaji wako.”
Rai hiyo ilitolewa katika kampeni ya uhamasishaji wa upimaji wa viashiria vya awali vya magonjwa ya figo, moyo, kisukari, na shinikizo la damu iliyofanyika kwa muda wa siku mbili kuanzia tarehe 22 hadi 23 januari 2021 huduma ambayo iliyotolewa bure bila malipo yoyote iliyofanyika chini ya udhamini wa kituo cha matibabu AFYA-POINT ikilichopo mtaa Mfaranyaki karibu na kituo cha daladala Buhemba Manispaa ya Songea.
Mganga mkuu Manispaa ya Songea Amosi Mwenda akiongea kwaniaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea, ambapo alitamka kuwa zoezi hilo limekuja wakati muafaka na wametumia fursa hiyo ya kupima viashiria vya awali vya magonjwa ya Figo, Moyo, Kisukari na Shinikizo la damu kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wenye matatizo kama hayo, na baada ya kupata vipimo kama watakuwa wamepta matatizo hayo watapata ushauri wa kitabibu na namna ya kuishi.
Halmashauri ya Manispaa ya Songea inatoa shukrani kwa Mkurugenzi wa kituo cha AFYA-POINT kwa kutoa huduma bure ya upimaji wa viashiria vya awali vya magonjwa ya Figo zoezi liliiofanywa na Wataalamu wa afya wa manispaa ya Songea chini ya Daktari bingwa wa magonjwa ya Figo pia kuunga mkono jitihada za Serikali kwa kutoa huduma bora za Afya. ” Mwenda alitamka”
Alitoa wito kwa wananchi wote kujitokeza kwenda kupima afya zao mara kwa mara ili waweze kuishi kwa kutambua zao. Kituo hicho ni kipya kinatarajia kuanza kufanya kazi ya kutoa huduma za matibabu hivi karibuni.
Alifafanua kuwa, miongoni mwa huduma itakayowapunguzia adha wagonjwa kusafiriri kwenda nje ya Mkoa ambayo hivi kwa sasa itapatikana katika kituo hicho ni pamoja na huduma za kusafisha damu ambayo kitaalamu huitwa “HEMODIALYSIS”.
Naye Mkurugenzi wa kituo cha AFYA-POINT Octavian Kassanga amebainisha kuwa kituo hicho kitatoa huduma za matibabu kufanya uzinduzi wa upimaji bure wa figo, moyo, kisukari na shinikizo la damu bure, kwa lengo la kubaini viashiria vya awali vya magonjwa ambayo yanaweza kuonekana kwa sasa au kujitokeza kwa baadaye.
Dr. Octaviani amesema kituo binafsi kimeweza kufadhili zoezi hilo kwa lengo la kuunga mkono jitihada za Serikali ili jamii iweze kubaini afya zao pia wawaze kujitambua kiafya kama wameathiriwa na maradhi hayo ili waweze kwenda kupata tiba nje ya Songea au katika kituo hicho.
Awali kituo hicho kilianza kufanya kazi 01 Octoba 2020 kwa kutibu magonjwa ya figo, na kuanzia taehe 25 januari 2021 baada ya kutimiza vigezo na masharti kituo hicho kitaanza kutoa huduma za matibabu kwa magonjwa mbalimbali pamoja na huduma ya kupumzisha.
Alisema baada ya kubaini uwepo wa wagonjwa wengi kutoka Mkoa wa Ruvuma ili ya kuwaondolea adha ya umbali wa huduma inakopatikana aliona heri afungue kituo cha tiba Songea kwa ajili ya kuwasogezea huduma za upimaji wa Figo, moyo, kisukari na shinikizo la damu ambapo alizindua huduma hiyo kwa kutoa vipimo bure kwa kila aliyefika kituoni hapo.
Katika kampeni hiyo ya upimaji iliyotolewa bure bila malipo kituoni hapo jumla ya watu 743 walipimwa na kati ya hao me 292na ke 451.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
AFISA HABARI MANISPAA YA SONGEA.
25.01.2021.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa