KiWANDA hiki cha kukoboa Mpunga cha MWEMBERIDHIKI kilichopo Kata ya Misifuni Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma, kilianza shughuli ya usindikaji wa Mpunga mnamo Disemba, 2017. Gharama za ujenzi wa kiwanda hiki ni Shilingi milioni 106 na gharama ya ununuzi na ujenzi wa mitambo ni Shilingi milioni 36 hivyo kufanya jumla ya gharama za uanzishaji wa kiwanda hiki kuwa shilingi milioni 142 .
Mmiliki wa kiwanda hiki ni Rashid Kangoma mkazi wa Wilaya ya Namtumbo,kiwanda hiki kimetoa ajira za kudumu kwa watu wawili ambao wote ni wanaume na za muda mfupi kwa watu 22 ambao wanawake wanne na wanaume 18. Mitambo na miundombinu iliyofungwa kwenye kiwanda hiki ina uwezo wa kukoboa Mpunga tani 24 kwa siku, lakini kwa sasa kinakoboa wastani wa tani tatuza Mpunga kwa siku. Kiwanda kinakoboa chini ya uwezo hii ni kutokana na upungufu wa upatikanaji wa malighafi ya mpunga.
Faida zinazopatikana kutokana na kiwanda hiki ni kama ifuatavyo;Kuongeza ajira katika Mkoa wa Ruvuma na watu kupata fursa ya kujiajiri wenyewe kwa kujikita katika kilimo cha mpunga kwani soko ni la uhakika,Upatikanaji wa soko la Mpunga la uhakika hivyo kuongeza kipato cha mkulima mmoja mmoja na hatimaye pato la Taifa,.Kuongeza pato la Taifa kwa kulipa kodi, leseni na ada ya TFDA,Upatikanaji wa Mchele safi na bora ikiwa mitambo ina uwezo wa kutenganisha mawe, chenga na uchafu.
Imetolewa na Albano Midelo
Afisa Habari wa Manispaa ya Songea
Juni 12,2016
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa