Mwenyekiti wa ccm mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho amewataka wananchi wa mkoa wa Ruvuma kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kupiga kura ili waweze kupata fursa ya kuchagua viongozi bora.
Ameyasema hayo katika ziara yake ya manispaa ya songea ambapo amewataka wananchi wa mkoa huo wa Ruvuma kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la kupiga kura na kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mtaa.
Akizungumza Mbunge wa viti maalumu mhe. Jacqueline msongozi ambapo amewahimiza akina mama wa mkoa wa Ruvuma kuendelea kuandaa lishe bora kwa watoto ili kutokomeza udumavu.
Ziara hiyo imefanyika katika Halmashauri zote 8 zilizopo mkoani Ruvuma ambapo itahitimishwa katika Manispaa ya songea kwa lengo la kutembelea matawi mbalimbali ya ccm na kuwahimiza mabalozi wa chama hicho kuendelea kujisajili wanachama wapya pamoja na kufanya vikao vya shina, na matawini.
Ziara hiyo imeanza tarehe 2 Septemba 2024 na inatarajia kukamilika tarehe 04 Septemba 2024.
Imeandaliwa na;
Amina Pilly;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa