Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanal. Laban Thomas amezindua kongamano la JIONGEZE ni zamu yako lililofanyika leo tarehe 15 Septemba 2023 katika ukumbi wa Manispaa ya Songea.
Kongamano hilo linalenga kutoa elimu ya kufungua fursa za sekta ya uchumi na uwekezaji Mkoani Ruvuma ambalo linaendeshwa na WASAFI Media, ambalo limeanza katika Mkoa wa Mtwara, Lindi na sasa Mkoani Ruvuma.
Katika kufanikisha kongamano hilo wameshirikisha wadau mbalimbali wakiwemo na wadau wa kilimo, Madini, Barabara “TARURA”, TANESCO, wanafunzi, wazee na wananchi mbalimbali kwa lengo la kufuangua fursa za uwekezaji Mkoani Ruvuma.
Imeandaliwa na;
Amina Pilly;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa