UMOJA wa Mataifa umetangaza rasmi kufanyika maadhimisho ya siku ya sokwe duniani kila mwaka ifika Julai 14 na Tanzania ikiwa ni moja ya nchi wanachama wa Umoja huo inaanza mwaka huu kutekeleza maadhimisho hayo.
Tukiwa tupo katika mwezi wa maadhimisho hayo,tutazama maisha ya sokwe ambayo utafiti umebaini kuwa yanafanana na maisha ya binadamu kwa asilimia zaidi ya 90.
Utafiti umebaini kuwa sokwemtu anabeba mimba kwa muda wa miezi nane na nusu.lakini pia ananyonyesha kwa muda wa miezi sita,binadamu wanachagua marais,lakini pia sokwe wanachagua marais wao ambao wanapatikana kwa kupigana ambapo sokwe anayeshinda ndiyo anakuwa kiongozi wa sokwe.
utafiti umeonesha kuwa, asilimia zaidi ya 96 ya chembe za urithi za binadamu zinafanana na zile za sokwe, pia ubongo wa sokwe na vitendo vyao vinafanana sana na vile vya binadamu.
Mhifadhi wa Hifadhi za Taifa (TANAPA) Noelia Mnyonga anasisitiza kuwa tafiti za kisayansi zimethibitisha kuwa Sokwe ni wanyama ambao wanafanana na binadamu katika tabia kwa asilimia 98 na kusisitiza kuwa ndiyo maana wanaitwa sokwe mtu.
“Sokwemtu ni mnyama ambaye alibakiza asilimia mbili tu angeweza kufanana na binadamu kitabia kwa asilimia 100 hali ambayo inamfanya mnyama huyu kutafutwa kwa udi na uvumba baada ya kuwa kivutio adimu na cha kipekee cha utalii duniani kote’’,anasema Mnyonga.
Mwandishi wa makala haya ni Albano Midelo
Afisa Habari Serikalini akiwa Songea mkoani Ruvuma
Mawasiliano albano.midelo@gmail.com,simu 0784765917
Julai 10,2018
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa