TAMASHA la kumbukizi ya Vita vya Majimaji na utalii wa utamaduni,hufanyika kila mwaka katika Makumbusho ya Taifa ya Majimaji. Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa ya Majimaji Balthazar Nyamusya anasema tamasha hilo litafanyika kwa siku tatu mwezi huu kuanzia Februari 25,26 na kilele chake kitakuwa Februari 27 . Tamasha hilo hufanyika kila mwaka mwezi Februari likiwa na lengo la kuwakumbuka mashujaa wa Tanzania waliopigana vita vya maji maji na kunyongwa na wajerumani Februari 27 mwaka 1906.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa