Kwa kupitia kifungu cha 4C cha sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Tume imepewa mamlaka ya kutoa elimu ya mpiga kura, kuratibu na kusimamia asasi na watu wanaotoa elimu hiyo.
Kauli hiyo imetamkwa na Jaji (MST) Mary H.C.S Longway wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau wa uchaguzi Mkoani Ruvuma wakiwemo na viongozi wa dini, wazee wa kimila, wawakilishi wa watu wenye ulemavu, wawakilishaji wa vijana, wawakilishi wa wanawake, wawakilishi wa asasi za kiraia, watendaji wa tume, na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Songea 01.10.2020.
Jaji Longway alisema “lengo la mkutano huo ni kutoa elimu ya mpiga kura kwa jamii pamoja na kuwashirikisha wadau kama watu wenye ulemavu waweze kushiriki katika mchakato wa uchaguzi kama inavyotamkwa kwenye Ibara ta 5 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977) kwamba kila raia wa Tanzania aliyetimiza umri wa miaka 18 anayo haki ya kupiga kura.”
Alibainisha kuwa pamoja na uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura ambao umewezesha daftari hilo na kuwa zaidi ya wapiga kura 9000 kwa Mkoa Ruvuma na jumla ya wapiga kura 29,188,347 kwa nchi nzima.
Aliwatoa hofu wapiga kura wote wenye mahitaji maalmu kwa kuwa maelekezo yametolewa kwa watendaji wa uchaguzi kutoa kipaumbele kwa watu wanaoishi na ulemavu, akina mama wanaonyonyesha, waliokwenda na watoto vituoni, wazee na wagonjwa pamoja na wajawazito.
Aliongeza kuwa kwa wale wasiojua kusoma na kuandika wanaruhusiwa kwenda na watu wanaowaamini kwa ajili ya kuwasaidia kupiga kura. Alisema kila kituo cha kupigia kura kutakuwa na kifaa cha maandishi ya nukta nundu ‘Tactile ballot folder’.
Alifafanua kuwa wenye ulemavu wa viungo vituturi vitakavyotumika kupigia kura vinaruhusu kuwahudumia kwa kugeuza kituturi kinakuwa kifupi na kumwezesha mwenye ulemavu wa viungo kupiga kura.
.
Mwisho alisema Tume itahakikisha uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 unakuwa huru, wa wazi, wa haki, na wa kuaminika kwa kuweka mazingira sawa ya ushindani kwa wagombea na vyama vyote vya siasa vinashiriki.
Nao wadau mbalimbali walioshiriki mkutano huo wakizungumza na kituo hiki ambapo walisema “tunaipongeza Tume ya Taifa ya uchaguzi kwa kutoa elimu kwa wadau na kushirikisha katika michakato ya kuelimisha jamii juu ya elimu ya mpiga kura.” Kumbuka uchaguzi mkuu wa mwaka huu wakuchagua Rais, Ubunge, na Madiwani unatarajia kufanyika 28 oktoba 2020.
IMETAYARISHWA NA;
AMINA PILLY;
AFISA HABARI MANISPAA YA SONGEA.
02.10.2020.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa