Mkoa wa Ruvuma una utajiri mkubwa wa utalii wa utamaduni ukilinganisha utalii wa ikolojia,miongoni mwa vivutio vya utalii wa utamaduni ni Makumbusho ya Taifa ya Majimaji yaliopo katika eneo la Mahenge Manispaa ya Songea.
Afisa Maliasili na Utalii wa Mkoa wa Ruvuma Afrikanus Challe anabainisha kuwa,wadau wa utalii katika Mkoa wa Ruvuma wamekusudia kuanzisha utalii wa kiutamaduni (cultural tourism) sanjari na kuboresha maeneo yote ya kihistoria ili kuendeleza utamaduni hatimaye maeneo hayo yaweze kuingiza mapato baada ya watalii kutembelea kama ilivyo katika visiwa vya Zanzibar.
Challe anasema,wadau kutoka wilaya zote za mkoa wa Ruvuma tayari wameshatembelea maeneo muhimu ya kihistoria kama vile Makumbusho ya Taifa ya Majimaji, Maposeni,Luhira na Chandamali katika Wilaya ya Songea ili kutambua maeneo ya kihistoria na umuhimu wake kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho.
Kwa upande wake Mjumbe wa Baraza la Makumbusho ya Majimaji Aidani Kabakuli anasema kila mwaka baraza hilo hufanya kumbukizi la kuwaenzi na kuwakumbuka mashujaa hao wakiwemo mashujaa 68 ambao walinyongwa na kuzikwa katika kaburi moja.
“Katika tukio la mashujaa hao kunyongwa walitimiza wajibu wao kwa ajili ya maslahi ya taifa letu la sasa na kizazi kijacho ambapo ushujaa ndiyo njia pekee ya kujikomboa na kulinda uhuru wa Taifa letu’’,anasisitiza Mteso.
Mwenyekiti huyo kwa niaba ya Baraza la Makumbusho ya Majimaji ameishukuru serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii kwa uamuzi wa kumiliki Makumbusho ya Taifa ya Majimaji ili kurithisha mila ,desturi na utamaduni kwa vijana wa sasa na vizazi vijavyo.
“Hali ya mila,utamaduni na desturi iliyopo kwa vijana wa sasa katika nchi yetu ni mbaya kwa kuwa vijana wengi wamesahau utamaduni mila na desturi za mtanzania na kuendekeza mila za kigeni ambazo zimeharibu kabisa maadili mema ya mtanzania’’,anasema.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa