PORI la Akiba la Liparamba lipo katika ukanda wa wa misitu maarufu duniani ya miombo woodland.Pori linakadiriwa kuwa na tembo zaidi ya 60,000 kulingana na utafiti ambao ulifanywa mwaka 2011.
Pori hilo linapita katika wilaya za Songea,Nyasa na Mbinga mkoani Ruvuma, lilikabidhiwa rasmi kwa Wizara ya Maliasili na Utalii chini ya usimamizi wa Idara ya Wanyamapori serikani Juni 5 mwaka 2006.Pori lina ukubwa wa kilometa za mraba 571 likiwa na eneo la kilometa za mraba 11,396.
Takwimu za Wizara ya Maliasili na Utalii za mwaka 2003 zinaonesha kuwa idadi ya tembo nchini iliongezeka na kufikia 120,000 ambapo nusu ya tembo hao walitoka katika pori la Akiba la Selous ambapo Liparamba ni ushoroba wa tembo toka Selous ambao wanavuka hadi nchini Msumbiji.
Hata hivyo sensa ya Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania(TAWIRI) ya mwaka 2009 ilionesha idadi ya tembo nchini ilikuwa 109,051 ambapo kutokana na kukithiri kwa ujangili mwaka 2014 idadi ya tembo ilishuka hadi kufikia 43,330 sawa na asilimia 60 ya tembo wote.
Kutokana na ukubwa wa misitu mizito minene iliyopo katika pori hilo inachangia kupunguza hewa ukaa(CO2).Liparamba ni eneo muhimu katika mchakato wa (Carbon sink) ambao hupokea mvua za kutosha kwa msimu mmoja tu kwa mwaka.Miongoni mwa vivutio adimu katika pori hili ni uoto wa asili, zikiwemo aina 60 za miombo,nyasi adimu aina 35,aina 80 za ndege na wanyama wa aina mbalimbali .wakiwemo tembo, simba, chui,parahali, tandala, pundamilia, nyati, kuro, pofu, kima, mamba,kiboko,ngiri na wanyama wengine.
pori hilo lina uoto wa asili ambao haujaharibiwa katika ukanda wa wilaya za Mbinga na Nyasa na kwamba pori hilo linatoa matunzo ya tembo wanaohamia kutoka Msumbiji na kuja Tanzania na kurudi Msumbiji na kwamba utafiti umebaini wanyama wengine wakifika Tanzania hawarudi Msumbiji.
Makala imeandikwa na Albano Midelo
Baruapepe:albano.midelo@gmail.com,simu 0784765917
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa