Hifadhi ya asili ya Luhira iliyopo mjini Songea ni moja ya kivutio adimu cha utalii kilichopo kilometa saba toka mjini Songea mkoani Ruvuma. Hii ndiyo hifadhi pekee ya asili katika nchi nzima iliyopo mjini .Ina wanyama wa aina mbalimbali wakiwemo pundamilia, nyani,mbawala, kakakuona, aina 105 za uyoga, nyoka wa aina mbalimbali wakiwemo chatu na ndege wa aina mbalimbali . Hifadhi hii ilianzishwa mwaka 1973 .
Hifadhi ya Luhira ina ukubwa wa hekta 600.Licha ya hifadhi hiyo kuwa na wanyama wa aina mbalimbali wakiwemo pundamilia, pongo, fisimaji, nyani, tumbili, kakakuona, kobe na chatu. Tozo ya kiingilio Raia wa Tanzania watu wazima sh.2000,watoto wenye umri kati ya miaka sita hadi 16 sh.500 na Watoto chini ya miaka sita ni bure
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa